Chama cha KANU kinamtaka mbunge wa Emurua Dikkir Johanna Ng’eno aliyeshtakiwa leo kwa tuhuma za uchochezi kujiuzulu kutoka chamani au afurushwe.
Katibu mkuu wa KANU Nick Salat anasema matamshi ya Ngeno yaliyoelekezwa kwa Rais Uhuru Kenyatta yanatamausha na kamwe chama hicho hakiungi mkono amiri jeshi mkuu kukosewa heshima.
Ngeno alikanusha tuhuma za uchochezi hii leo katika mahakama ya Nakuru na kufungiwa hadi Alhamisi wiki hii wakati mahakama itatoa uamuzi wa ombi lake kutaka kuachiliwa kwa dhamana.