Omar Boga ni maarufu Msambweni wasema utafiti

0

Omar Boga wa chama cha ODM angeibuka mshindi kwenye uchaguzi mdogo wa Msambweni iwapo zoezi la uchaguzi lingeandaliwa leo umebaini utafiti wa kampuni ya TIFA.

Kampuni hiyo inasema Boga angepata asilimia 54% ya kura zote huku mgombea huru Feisal Abdalla akiibuka wa pili na asilimia 29%

Wawaniaji wengine Ali Hassan Mwakulonda na Mwarere Mwachai wangepata asilimia 9% na 2% mtawalia kwa mujibu ya utafiti huo.

Utafiti huo vile vile umoenesha kuwa chama cha ODM ndicho maarufu sana katika eneobunge hilo kwa asilimia 48% kikifuatiwa na Jubilee kwa asilimia 24%.

Utafiti huo ulifanywa kati ya Jumapili na Jumanne wiki hii ambapo watu 320 walihojiwa.

Uchaguzi mdogo wa Msambweni unatazamiwa kufanyika tarehe kumi na tano mwezi huu kufuatia kifo cha Suleiman Dori.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here