Omar Idd Boga ameshinda zoezi la mchujo la chama cha ODM na sasa atapeperusha tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni.
Boga ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 6,183 dhidi ya mshindani wake wa karibu Nicholas Zani aliyejizolea 530.
Boga sasa atamenyana na wagombea wengine 10 katika uchaguzi huo mdogo utakaondaliwa Disemba 15.
Chama cha Jubilee kilitangaza kujiondoa katika uchaguzi huo kutokana na handisheki baina ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga.