ODM yafanyia bodi ya uchaguzi mabadiliko

0

Profesa Catherine Mumma ndiye mwenyekiti mpya wa bodi ya uchaguzi katika chama cha ODM kwa muda wa miaka mitano ijayo.

Kamati ya uongozi ya chama hicho imeafikia uamuzi huo kwenye mkutano ulioongozwa na kiongozi wa chama hicho Raila Odinga.

Wanachama wengine wa bodi hiyo ya uchaguzi ni Abdulahi Diriye, Richard Tairo, Syntei Nchoe na Emily Awita.

Kamati ya nidhamu chamani itaongozwa na Profesa Ben Sihanya, wanachama wakiwa ni Ramadhan Abubakar, Mumbi Ngaru, Seth Kakusye na Dkt. Florence Omosa.

Kibarua cha kwanza kwa bodi hiyo ya uchaguzi ni maandalizi ya chaguzi za mashinani kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here