ODM watakiwa kuharakisha mchakato wa kumuondoa Obado

0

Chama cha ODM kimetakiwa kiharakisha mchakato wa kumng’oa gavana wa kaunti ya Migori Zachary Okoth Obado baada yake kushtakiwa kwa ufisadi.

Baraza kuu la vijana kutoka kaunti hiyo ya Migori likiongozwa na Julius Omamba linataka gavana huyo kuondoka mara moja ili kuondoa hali ya sintofahamu inayowakumba wakaazi kuhusu hatma yake.

Kauli hizi zinajiri baada ya chama hicho kuidhinisha  kuondolewa kwa gavana huyo kupitia kuwasilishwa kwa mswada wa kutokuwa na imani naye.

Obado alishtakiwa kuhusiana na sakata ya ufujaji wa Sh73M na kuzuiliwa kuingia afisini hadi kesi dhidi yake ikamilike.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here