Viongozi wakuu wa chama cha ODM hii leo wanatazamiwa kuandaa kikao na waakilishi wadi wa chama hicho katika bunge la kaunti ya Migori, siku moja baada ya mahakama kumzuia Gavana Okoth Obado kuingia afisini.
Katika barua kwa kiranja wa wengi kwenye bunge hilo Keke Oyugi, mkurugenzi mkuu wa ODM Oduor Ongweny amewataka MCAs hao kufika katika makao makuu ya chama hicho hii leo .
Haijabainika wazi ajenda ya mkutano huo lakini katibu mkuu Edwin Sifuna amekanusha ripoti kuwa wanapanga kumbandua afisini Obado.
Hiyo jana, Obado alipata pigo baada ya mahakama kumuagiza asiingia katika afisi yake hadi pale kesi ya ufisadi inayomkabili itakaposkizwa na kuamuliwa.
Waakilishi wadi wa Kiambu walimtimua aliyekuwa Gavana Ferdinand Waititu baada yake kushtakiwa kwa tuhuma za ufisadi na kuzuiwa pia kuingia afisini.