ODM, Jubilee wagawana viti bungeni

0

Mbunge wa Moiben Silas Tiren amechaguliwa bila kupingwa kuwa mwenyekiti mpya wa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu Kilimo na wadhifa uliokuwa unashikiliwa na mwenzake wa Mandera Kusini Adan Ali.

Ali ni miongoni mwa wabunge 16 wendani wa naibu rais William Ruto waliotimuliwa kwenye uongozi wa kamati mbalimbali za bunge.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Laikipia Catherine Waruguru amechaguliwa kuwa naibu mwenyekiti wa kamati hiyo nafasi anayoichukua kutoka kwa mbunge wa Navakholo ni kiranja wa bunge hilo Emmanuel Wangwe.

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo amechaguliwa kuwa naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge hilo kuhusu haki na maswala ya kisheria, mwenyekiti wake akiwa mwenzake wa Kangema Muturi Kigano wote wakichaguliwa pasipo kupingwa.

Kamati ya elimu itaongozwa na mwakilishi wa akina mama kaunti ya Busia Florence Mutua, naibu wake akiwa ni mbunge wa Nyeri Ngujiri Wambugu.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Homa Bay Gladys amechaguliwa mwenyekiti mpya kamati ya bunge kuhusu fedha, naibu wake akiwa mbunge wa Roysambu Waihenya Ndirangu.

Mbunge wa Limuru Peter Mwathi na mwenzake wa Chepalungu Gideon Koskei watahudumu katika kamati ya bunge kuhusu Leba kama mwenyekiti na naibu wake mtawalio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here