Huku mjadala kuhusu mswada wa ugavi tata wa mapato ukitazamiwa kurejea bungeni wiki hii, kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amewasuta maseneta wanaopinga mswada huo licha ya kwamba kaunti zao zitapata mgao mkubwa wa fedha.
Akizungumza mjini Kakamega anapoendelea na ziara za kukutana na viongozi wa mashinani, kiongozi huyo wa chama cha ODM ameonekana kumlenga seneta wa Kakamega Cleophas Malala ambaye yuko katika kundi la maseneta wanaopinga mfumo utakaozingatia idadi ya watu kugawa pesa.
Odinga akiwa ameandamana na mwenyeji wake na naibu kiongozi wa chama hicho Wycliffe Oparanya vile vile amepigia debe ripoti ya BBI ambayo inatazamiwa kutolewa hivi karibuni.
Ikumbukwe kwamba baraza la magavana limetishia kuwatuma nyumbani wafanyikazi wake Septemba 17 kwa kukosa pesa iwapo utata huo uliopo kuhusu mswada wa ugavi wa mapato hautatanzuliwa.