Odinga ampongeza rais Kenyatta kwa kutatua mgogoro kuhusu mgao wa fedha

0

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amepongeza juhudi zilizowekwa na rais Uhuru Kenyatta katika kutanzua utata uliokuwa unazingira mswada wa ugavi wa mapato.

Odinga katika taarifa amefafanua kuwa rais Kenyatta alisaidia kutatua mgogoro huo uliotatiza shughuli katika serikali za kaunti alipoahidi kutoa Sh50b kwa serikali za kaunti kipindi kijacho cha matumizi ya pesa za serikali.

Kinara huyo wa ODM vile vile amesifia hatua ya bunge la Senate kutumia ahadi hiyo ya rais kutanzua mgogoro huo uliosababisha magavana kusitisha shughuli muhimu katika serikali za kaunti.

Hata hivyo waziri huyo mkuu wa zamani amewasuta baadhi ya viongozi anaosema walitaka kutumia mgogoro huo kujitafuta umaarufu wa kisiasa akisema ni Wakenya walioshinda na wala sio mwanasiasa yeyote.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here