Odinga aelekea DR Congo kwa ziara ya siku mbili

0

Mwakilishi Mkuu wa miundo msingi katika muungano wa AU Raila Odinga ameondoka nchini kueleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ziara ya siku mbili.

Katika taarifa, msemaji wa Odinga Dennis Onyango amesema waziri huyo mkuu wa zamani ameratibiwa kufanya mkutano na mwenyeji wake Rais Felix Tshisekedi kuhusiana na hatua zilizopigwa katika ujenzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Inga.

Odinga anatazamiwa kupigia debe mradi huo unaoendeshwa na Congo kama mradi wa bara la Afrika kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here