Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga amepeleka kampeni zake za kusaka Uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) nchini Algeria.
Raila amekutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nadir Larbaoui, ambapo walijadiliana naye mipango yake kwa bara la afrika, iwapo atachaguliwa kama mwenyekiti wa AUC.
“Nimepokelewa kwa furaha mjini Algiers, na Mh. Nadir Larbaoui, Waziri Mkuu wa Algeria. Tumekuwa na fursa ya kujadili uhusiano wetu kama nchi ndugu.
“Nilimuelezea maono yangu kwa Umoja wa Afrika na haja ya kuimarisha zaidi a ustawi wa bara letu. Asante Waziri Mkuu,” Raila amesema kwenye X.
Mapema wiki hii Raila alipeleka kampeni zake Kusini mwa Afrika akikutana na Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, Rais wa maozabique Daniel Chapo na Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe.
Raila anakabiliana na Mahamoud Youssouf wa Djibouti katika kinyanganyiro cha kuwania nafasi hio.
Odinga tayari amepata uungwaji mkono wa mataifa 23 ikiwa ni pamoja na Algeria, Angola, Botswana Burundi , Central African Republic, Congo, Democratic Republic of the Congo, Equatorial Guinea.
Mengine ni pamoja na The Gambia, Ghana, Guinea-Bissau, Malawi, Mauritius, Nigeria,Rwanda, Seychelles, South Sudan, Tanzania, Togo, Uganda, Zambia, Zimbabwe.
Uchaguzi wa AUC unatarajiwa kuandaliwa mwezi ujao.