Obado na wanawe waachiliwa kwa Ksh 16.25M

0

Gavana wa Migori Okoth Obado na wanawe wanne wameachiliwa kwa shilingi million kumi na sita nukta mbili tano baada ya kukana mashtaka ya kushirikiana kuiba pesa za umma.

Hakimu mkuu wa Mahakama ya Milimani Lawrence Mugambi ameagiza Obado kuachiliwa kwa shilingi million 8.7 pesa taslimu huku wanawe Ocholla, Scarlet, Jerry na Everline wakiachiliwa na kati ya shilingi million mbili na shilingi million tatu pesa taslimu.

Washukiwa wengine sita Jared Odoyo, Christine Ocholla, Joram Otieno, Patroba Otieno, Penina Auma na Caroline Anyango wameachiliwa kwa kati ya shilingi million nane nukta tano na shilingi million mbili.

Inadaiwa kuwa washukiwa walishirikiana na kuiba shilingi million 73.4 pesa za kaunti ya Migori.

Wakati uo huo Gavana wa Migori Okoth Obado amepata pigo baada ya mahakama kumuagiza asiingia katika afisi yake hadi pale kesi ya ufisadi inayomkabili itakaposkzwa na kuamuliwa.

Katika uamuzi wake, hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Lawrence Mugambi badala yake ameagiza Obado kupelekwa na maafisa wa polisi kuondoa vitu zake za kibinafsi.

Obado sasa ni Gavana wa nne kuzuiwa kuingia afisini kutokana na tuhuma za ufisadi, magavana wengine wakiwa Mike Sonko wa Nairobi, Moses Lenolkulal wa Samburu na aliyekuwa Gavana wa Kimabu Ferdinand Waititu.

Obado, wanawe wanne na washukiwa wengine wamelazimika kukeshakorokorni tangia siku ya Alhamisi walipofunguliwa mashtaka.

Naibu Gavana wa kaunti ya Migori Nelson Mahanga ametetea Obado kuhusina na madai dhidi yake na kusema pesa zinazodaiwa kupotea si pesa za kuwashtua wakaazi wa Migori na ambazo zinaweza kusabbaisha miradi ya maendeleo kukwama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here