‘Obado lazima angatuke’ – ODM

0

Chama cha ODM kinashikilia kuwa Gavana wa Migori Okoth Obado lazima angatuke madarakani baada yake kushtakiwa kwa tuhuma za kuiba shilingi million 73 pesa za mlipa ushuru.

Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho hii leo, mwenyekiti wa kitaifa chama hicho John Mbadi anasema kuzuiliwa kwa Obado kuingia afisini kunawanyima wakaazi huduma muhimu.

Nao viongozi wa chama hicho cha Chungwa eneo la Migori wanawataka waakilishi wadi kuharakaisha mchakato wa kumbandua afisini Gavana Obado na naibu wake Nelson Mahanga Mwita kuapishwa kuendelea na majukumu.

ODM sasa inataka waakilishi wadi wanaounga mkono kutimuliwa kwa Obado kupewa ulinzi zaidi baada ya kudai kuwa wamekuwa wakipokea vitisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here