Obado kutetewa na baadhi ya MaMCA

0

Baadhi ya wawakilishi wadi wanaonuia kumtetea gavana wa Migori Zachary Okoth Obado wanapanga kukutana.

MaMCAs hao wanakutana huko Kuria kupanga mikakati watakayoweka kumuokoa gavana huyo aliyezuiliwa na mahakama kuingia afisini baada ya kushtakiwa kwa ufisadi.

Haya yanajiri siku moja baada ya chama cha ODM kupitia kwa mwenyekiti wake John Mbadi kishikilia kuwa ni lazima Obado ang’atuke afisini baada yake kushtakiwa kwa tuhuma za kuiba shilingi million 73 pesa za mlipa ushuru.

Nao viongozi wa chama hicho cha Chungwa Migori wanawataka waakilishi wadi kuharakakisha mchakato wa kumbandua afisini Gavana Obado na naibu wake Nelson Mahanga Mwita kuapishwa kuendelea na majukumu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here