Ngwele akatazwa kuingia afisini

0

Mahakama imetoa agizo linalomzuia karani wa bunge la kaunti ya Nairobi Jacob Ngwele dhidi ya kuingia afisini hadi kesi dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Jaji Maureen Onyango wa mahakama ya Leba badala yake imemuagiza naibu wake Adah Onyango kuchukua majukumu ya kuwa karani hadi uamuzi kwenye kesi hiyo utakapotolewa mwezi Oktoba

Aidha, mahakama hiyo imebatilisha uteuzi wa Edward Gichana kuchukua wadhifa huo baada yake kuapishwa na spika Beatrice Elachi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here