Nge’no kulala seli siku mbili zaidi

0

Mbunge wa Emurua Dikkir Johanna Kipyegon Nge’no atakesha korokoroni kwa muda wa siku mbili akisubiri uamuzi wa ombi la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Hii ni baada yake kufikishwa katika mahakama ya Nakuru na kukanusha mashtaka ya uchochezi aliyotoa kumhusu Rais Uhuru Kenyatta na uhifadhi wa msitu wa Mau.

Upande wa mashtaka umeiambia mahakama kuwa matamshi hayo yana uwezo wa  kusababisha uhasama miongoni mwa jamii zinazoishi kaunti ya Narok.

Ngeno alikamatwa jana usiku nyumbani kwake Mogondo, eneo la TRanmara na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Nakuru Central.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here