Nelson Havi aishtumu serikali kwa kuingilia shughuli za LSK

0

Rais wa chama cha mawakili nchini LSK Nelson Havi sasa anadai kuwa serikali inamtumia afisa mkuu mtendaji Mercy Wambua kama kibaraka chake kuvuguruga shughuli za chama hicho.

Havi katika mkutano na waandishi wa habari amedai kuwa licha ya kumtimua afisini, Wambua amedinda kuondoka huku serikali ikimpa ulinzi.

Rais huyo wa LSK anasisitiza kwamba hatua yake ya kumkufuza Mercy Wambua ilikuwa ni kutoa nafasi ya kufanyika kwa ukaguzi kuhusu matumizi ya pesa za chama hicho anazosema zimeibwa.

Itakumbukwa kwamba baraza kuu la chama hicho lilipiga kura kupinga hatua ya kufutwa kazi kwa Wambua kwa misingi kwamba hakupewa nafasi ya kujitetea na kuagiza arejeshwe kazini mara moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here