Nation Media Group watetewa na MCK

0

Baraza la vyombo vya habari (MCK) limekosoa vitisho kutoka kwa magavana dhidi ya kampuni ya Nation Media Group kwa kuwaangazia magavana wanaofuatwa na tuhuma za ufisadi.

Baraza la magavana kupitia mwenyekiti wake Wycliffe Oparanya limetishia kutofanya matangazo na shirika la Nation kwa kuwaangazia magavana wanane wanaoandamwa na madai ya ufisadi mpaka waombwe msamaha.

MCK kupitia kwa taarifa iliyotumwa na afisa mkuu mtendaji David Omwoyo imetaja hatua hiyo kama tishio kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Ikumbukwe kwamba afisa mkuu mtendaji wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC Twalib Mbaraka aliambia bibliahusema.org kwamba  magavana kadhaa wanachunguzwa kwa madai ya kuhusika na wizi wa mali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here