Serikali imetangaza marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa moja za jioni hadi saa moja asubuhi huko Njoro, kaunti ya Nakuru kufuatia kuibuka upya kwa mapigano.
Mshirikishi wa eneo la bonde la ufa George Natembeya ametangaza kuanza kwa kafyuu katika maeneo ya Mariashoni, Ndoswa, Nessuit, Kaprop na Kapnoswa.
Natembeya amesema kuwa serikali imewatuma maafisa zaidi wa usalama kuhakikisha kuwa hali ya utulivu inarejea katika maeneo hayo.
Ameongeza kuwa watakaodhubutu kukaidi marufuku hiyo ya kutotoka nje watakamatwa na kushtakiwa.