NARC KENYA YAJIONDOA KIRASMI KUTOKA KWA MUUNGANO WA AZIMIO ONE KENYA

0

Wajumbe wa Kitaifa wa chama cha NARC Kenya Wameidhinisha kujiondoa kwa chama hicho kutoka kwa muungano wa Azimio la Umoja one Kenya baada ya muda wa notisi ya siku 90 uliotolewa kukamilika.

Chama hicho kimejiondoa kwenye muungano huo baada ya chama cha ODM kujiunga na Serikali Pana yaani broadbased Government inayoijumuisha na Chama ch UDA.

Kinara wa NARC Kenya Martha Karua amesema malengo na maono ya muungano wa Azimio iliyovutia chama cha Narc Kenya imegeuka baada ya vigogo wake kujihusisha na Rais William Ruto.

“Tuliingia kwenye Azimio kukomboa wakenya, wakati ambapo malengo ya Azimio yaligeuka, NARC Kenya ilitoa ilani ya nia ya kujiondoa.” Amesema Martha Karua.

“Siku tisini zimekamilika, tutamkumbusha msajili wa vyama vya kisiasa na hivi karibuni mutaona tukishereka tukiondoka Azimio” .

Wajumbe wa NARC Kenya aidha wameishinisha mpango wa chama hicho kusaka uongozi wa taifa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.

Miongoni mwa mipango iliyoidhinishwa ni mageuzi makuu ya chama hicho ikiwemo mageuzi ya Nembo na hata jina la chama inapojitayarisha kwa kampeni za 2027.

NARC Kenya imesema kuwa itafanya usajili wa wanachama wapya ili kujiimarisha kutoka ngazi ya mashinani na kuongeza ushawishi wake uchaguzi mkuu unapodogea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here