Tume ya EACC imemtaka Naibu Chansela wa Chuo Kikuu Cha Moi Issac Kosgey kufika mbele yake kujibu maswali kusiana na madai ya ufisadi uliokithiri katika taasisi hiyo ya elimu ya juu.
Meneja wa EACC Kanda ya Bonde la Ufaa Charles Rasugu amethibitisha kwamba Kosgey ametakiwa kufika mbele ya tume hiyo katika afisi zake jijini Eldoret Jumatano wiki hii.
Wito huo unakuja wakati ambapo kuna tuhuma za ufisadi kukithiri katika chuo hicho ambacho kina madeni ya zaidi ya Sh Bilioni 20 zikiwemo Bilioni 12 zinazodaiwa na wahadhiri walio kwenye mgomo.
“Tayari ameshapewa wito wa kufika kwa kuchomwa moto”, amesema Rasugu.
Rasugu ameongeza kwamba mameneja wengine kadhaa wa chuo hicho kikuu pia wametakiwa kuandikisha taarifa na tume hiyo.
Msemaji wa EACC Erick Ngumbi amedhibitisha kuwa tume hiyo itatoa ripoti ya kina kuhusu uchunguzi wake katika chuo kikuu.
“Tutatoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo”, amesema Ngumbi.
Tayari mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Nancy Gathungu ametoa onyo kuwa huenda taasisi hiyo ikanguka kutokana na mzigo mzito wa madeni.
Tawi la Chuo hicho ya Chama cha wahadhiri UASU limemtaka Profesa Kosgey kuondolewa afisini kwa kile wahadhiri wametaja kama usimamizi mbaya.
Ikumbukwe chuo hicho kilichukulia upanzi wa matunda aina ya tufaha kwenye shamba la ekari 1000 kama njia mbadala ya kupata mapato.