Nafuu kwa Sonko, mahakama ikimuokoa dhidi ya kubanduliwa

0

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amepata afueni ya muda baada ya mahakama kuhairisha mchakato wa kumwondoa afisini.

Akitoa agizo hilo, jaji Nzioki Makau ameagiza bunge la kaunti ya Nairobi kutoendelea mbele na vikao vya kujadili hoja ya kutokuwa na Imani na Gavana huyo hadi pale kesi aliyowasilisha itakaposkizwa na kuamuliwa.

Kwenye kesi hiyo, Sonko anasema mchakato huo wa kutaka kumwondoa afisini unaenda kinyume na maagizo ya mahakama kwani kuna kesi sawia na hiyo mahakamani.

Sonko alitakiwa kufika mbele ya bunge hilo Alhamisi wiki hii kujitetea kwa tuhuma za ufisadi na utumzii mbaya wa afisi kwenye hoja hiyo ya kutokuwa na imani naye iliyowasilishwa na kiongozi wa wachache Michael Ogada.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here