MWENYEKITI WA SAVVANAH CLINCKER WACHILIWA NA MAHAKAMA

0

Mahakama ya Hakimu imeamuru kuachiliwa bila masharti kwa Mwenyekiti wa Savannah Clinker Benson Ndeta baada ya kufahamishwa kuhusu agizo la mahakama kuu lililotolewa kusitisha kufunguliwa mashtaka na kuzuiliwa kwa mfanyIbiashara huyo.

Ndeta alikesha rumande wikendi nzima licha ya agizo la Mahakama Kuu lililotolewa Ijumaa iliyopita.

Ndeta Ijumaa iliyopita alishtakiwa kwa kuilaghai benki ya ABSA dola milioni 35 (Ksh.4.5 bilioni), akidaiwa kuchukua fedha hizo kama mkopo kwa niaba ya Savannah Cement Limited.

Mfanyibiashara huyo alishtakiwa kwa makosa manane kati yazo ikiwa ni kula njama ya kutenda uhalifu na kupata mkopo kwa njia za uongo madai aliyoyakana.

Ndeta ambaye alikamatwa jijini Nairobi pia amekanusha mashtaka ya kutengeneza hati bila mamlaka na kutoa stakabadhi za uongo.

Kupitia kwa wakili wake Cecil Miller, mfanyibiashara huyo ambaye pia ameonyesha nia ya kununua Bamburi Cement alijitetea akisema madai yanayomkabili ni njama ya kumnyima nafasi ya kununua kampuni hio.

Hakimu Gilbert Shikwe amehairisha uamuzi wa ombi la mshukiwa kuwachiliwa kwa dhamana na kuamuru kesi hiyo itajwe Januari 30, 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here