Asha Langoni, bintiye aliyekuwa mbunge wa Changamwe marehemu Ramadhan Seif Kajembe amezikwa Alhamisi chini ya masharti makali ya kuwapumzisha watu waliofariki kutokana na corona.
Marehemu aliyefariki Jumatano usiku katika hospitali ya Pandya amezikwa karibu na wazazi wake katika eneo la Kwashee Mikindani eneo bunge la Jomvu.
Kifo cha Langoni kinawadia chini ya majuma mawili baada ya Ramadhan Kajembe, 75, kufariki.
Langoni hakuhudhuria mazishi ya marehemu babake kwani alikuwa hospitalini akipigania maisha yake baada ya kuugua.
Aidha, familia hiyo ilimzika mkewe mbunge huyo wa zamani mazishi ambayo hakuhudhuria kwani alikuwa hospitalini.