ROBERT KIPKORIR Tanui mwanaume mwenye umri wa miaka 34 kutoka kijiji cha Seanin kaunti ya Bomet anazuiliwa katika kituo cha polisi akisubiri kufikishwa mahakamani Jumatano baada ya kumchoma mkewe Emmy Chepkoech Mitey ambaye ni naibu mwalimu mkuu wiki moja iliyopita.
Mshukiwa amekuwa mafichoni na maafisa wa idara ya upelelezi DCI wanasema wamemshika katika barabara ya Kisumu-Kericho akitaka kuabiri gari kuelekea kusikojulikana.
Inaarifiwa kuwa marehemu alikuwa ameaondoka nyumbani kwake kufuatia ugomvi wa kinyumbani kati yake na mumewe na kutorokea nyumbani kwa babake.
Wiki moja baadaye mumewe alimtafuta nyumbani kwa baba yake Seanin ambapo alimchoma kwa kutumia petrol.
Mitey hakuponea kwani alichomeka mwili wake wote licha ya familia yake kujaribu kuokoa maisha yake alipelekwa katika hospitali ya kimisheni Litein.
Licha ya madaktari kujaribu kadri ya uwezo wao hatimaye Mitei alikata roho.
Aidha familia ya mwendazake imedhibitisha kuwa Tonui amekua Mtu wa vurugu katika ndoa yake kila mara.
Haya yanajiri huku utafiti uliofaonywa na shirika la TIFA ukionesha kuwa visa vya dhulma za kinyumbani vimeongezeka wakati huu wa covid 19 katika maeneo ambapo watu wanapata kipato cha chini.
Kwa mujibu wa TIFA, aslimia 44% ya wanawake wamekandamizwa ikilinganishwa na aslimia 29% ya wanaume.
Asilimia 35% ya watoto wameathirika na dhulma hizo za kinyumbani.
Utafiti huo ulifanywa jijini Nairobi katika maeneo ya Kibra, Mathare, Kawangware na Mukuru kwa Njenga Septemba 24 na Octoba 2 mwaka huu.