Mwanasiasa wa upinzani Tanzania atafuta hifadhi Kenya akihofia maisha yake

0

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International limepinga vikali mipango ya serikali ya Kenya kumrudisha kwao mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema alikimbilia nchini jana kutafuta hifadhi akihofia maisha yake.

Katika taarifa, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo nchini Irungu Houghton anasema hatua hiyo ni kinyume na mikataba ya kimataifa ambayo Kenya imetia saini kuwapa hifadhi wakimbizi ambao wanatoroka makwao iwe kisheria au kinyume cha sheria.

Irungu anasema mwanasiasa huyo aliyekamatwa katika mpaka wa Namanga jana pindi baada ya kuvuka nchini ana haki kisheria ombi lake la kutafuta hifadhi nchini kuskizwa.

Shirika hilo linasema kumrudisha kwao Lema ni kukiuka haki zake za kibinadamu kwani yuko hatarini kukamatwa nchini humo na haki zake kukiukwa hata zaidi na serikali ya John Pombe Joseph Magufuli.

Lema alikamatwa baada ya uchaguzi mkuu uliopita ambapo Magufuli alitangazwa mshindi, kabla ya kuachiliwa bila kufunguliwa mashtaka yoyote.

Haya yanajiri huku kiongozi wa chama cha Chadema, Tundu Lissu akitafuta hifadhi katika makazi ya balozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam tangu siku ya Jumatatu.

Lissu amedai anahofia usalama wake baada ya kupokea ujumbe wa vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana wakiahidi ”kumshughulikia”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here