Mwanamke mmoja amewasilisha kesi mahakamani akitaka kusitisha mazishi ya mbunge wa Matungu Justus Murunga.
Agnes Wangui kupitia kwa wakili wake Danstan Omari anataka wajane wawili wa marehemu Christabel na Grace wazuiliwe kuongoza mazishi ya mwenda zake kwa sababu yeye na marehemu walikuwa wapenzi.
Mwanamke huyo anadai kuwa marehemu alikuwa mpenziwe na wamezaa naye watoto wawili na anataka uchunguzi wa DNA ufanywe kudhibitisha madai hayo.
Kimsingi, Wangui anataka yeye na wanawe wawili kuhusishwa kikamilifu katika safari ya mwisho ya marehemu sawa na kugawa mali yake.