MWANAMKE AKANYAGWA NA NDOVU AKITAFUTA KUNI

0

Mwanamke mmoja amekanyagwa na ndovu hadi kufa katika mbuga ya kitaifa ya Wanyama ya Amboseli, kaunti ya Kajiado, wakati akitafuta kuni.

Katika taarifa, shirika la wanyamapori KWS linasema mwanamke huyo alikuwa na mwenzake jana, tarehe kumi Machi 2020, mbugani humo wakitafuta kuni wakati mkasa huo ulitokea.

Katika taarifa, kaimu mkurugenzi wa mawasiliano wa KWS Ngugi Gecaga anasema walipokea taarifa kutoka kwa mwenzake lakini hawakufaulu kumwokoa.

Mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Loitoktok.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here