Wizara ya mambo ya nje nchini Kenya inasema mwanahabari aliyekamatwa nchini Ethopia Yassin Juma yuko huru.
Kupitia kwa mtandao wa Twitter, wizara hiyo inasema mwanahabari huyo kwa sasa amewekwa kwenye kituo cha karantini baada ya kupatikana na ugonjwa wa corona akiwa gerezani.
Baraza kuu la vyombo vya habari MCK kupitia afisa mkuu mtendaji David Omwoyo linasema limeiiandikia wizara hiyo ya maswala ya kigeni kutaka mwanahabari huyo kuachiliwa huru na kurejeshwa nyumbani.
Aidha Omwoyo ameelezea kuwa mwanahabari huyo amezuiliwa kwa muda mrefu kutokana na utaratibu ambao unahusisha mataifa mawili.
Juma amekuwa akizuiliwa kwa muda wa karibia miezi miwili sasa licha ya mahakama na mwanahseria mkuu nchini kuagiza awachiliwe.