Mwanahabari wa Kenya Yassin Juma amepona ugonjwa wa corona na yuko huru kurejea nyumbani baada ya kuachiliwa na Polisi nchini Ethopia.
Yassin Juma alikutwa na virusi hivyo alipokuwa anazuiliwa na Polisi baada ya kukamatwa.
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani imearifu kuwa Juma ameondoka hospitalini baada ya wito kutoka kwa Wakenya na mazungumzo baina ya mataifa yote mawili.
Juma hata hivyo anaarifiwa kuamua kusalia mjini Addis Ababa na rafiki zake kabla ya kuamua kurudi Kenya.