MWANAHABARI MWINGINE MASHUHURI AAGA DUNIA

0
SHADRACK MITTY
SHADRACK MITTTY

Sekta ya Uanahabari humu nchini imegubikwa tena na majonzi kufuatia kuaga kwa ripota wa Shirika la Standard Shadrack Miti.

Miti anaripotiwa kuugua kwa muda na ameaga usiku wa kuamkia Jumatano akiwa anapokea matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Kenyatta.

Miti alikuwa Ripota wa maswala ya Elimu akiripoti baadhi ya mabadiliko katika sekta hio ikiwemo mtaala wa Umilisi.

Naibu Mhariri wa Matangazo ya Standard Group Ken Mijungu amemkumbuka Mitty kama mtu mwenye “kujitolea sana na alizingatia viwango vya juu vya kitaaluma kazini.”

Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (KNEC) limesifu Mitty, likisema, “Ni kwa masikitiko makubwa tumesikia kuhusu kifo cha Shadrack Mitty wa KTN News. Mitty alikuwa mwanahabari mahiri ambaye kila mara aliripoti kwa ufasaha na kuarifu kuhusu masuala ya elimu.”

Hapo awali Mitty alihudumu chini ya QTV kwa miaka 5 ambapo alifanya kazi kuanzia 2012 hadi 2016 kabla ya kuhamia Standard Group.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here