Mwanafunzi wa kidato cha tatu anaarifiwa kuwadunga visu walimu wake wawili katika shule ya upili ya Kisii.
Mwalimu mmoja Edwin Mokaya alikuwa anamtaka mwanafunzi huyo kuelezea ni kwa nini alifika shuleni kuchelewa.
Hata hivyo mwanafunzi huyo alichukua kisu na kisha kumdunga mwalimu huyo kwenye paja la kichwa, mgongoni na miguuni.
Mwalimu mwingine Elvis Maoto aliyejaribu kuingilia kati pia alidungwa kisu kabla ya walimu wengine kufaulu kumkabili mwanafunzi huyo.
Walimu hao wawili walikimbizwa katika hospitali ya Ram kaunti ya Kisii kwa matibabu.