Mwanafunzi alilia haki baada ya kuchapwa na mwalimu – Eldoret

0

Mwanafunzi mmoja wakike kutoka shule moja ya upili iliyoko mjini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu anauguza majeraha katika hosipitali moja eneo hilo baada ya kudaiwa kuchapwa na kujeruhiwa na mwalimu wake wa somo la Kiingereza.

Inaarifiwa msichana huyo alipokea kichapo hicho kwa  kukosa kuvalia sare rasmi za shule.

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo Gitonga Mbaka amekiri kupokea lalama hizo na kuahidi kuwa uchunguzi wa kina utafanywa na hatua kuchukuliwa.

Mamake msichana huyo amekiri kuwa bintiye alienda shuleni bila sare rasmi kwani hakuwa na pesa za kumnunulia bintiye sare baada ya kulipa karo na sasa anataka haki kwa bintiye.

Hata hivyo Mwalimu huyo amekana madai dhidi yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here