Kenya imerekodi visa vipya 544 vya ugonjwa wa corona na kufikisha idadi ya visa hivyo kuwa 22, 597.
Katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema idadi hiyo imeongezeka baada ya kupima sampuli 2,653 katika muda wa saa Isirini na nne zilizopita.
Marian Awuor Adumba, 32, na muuguzi katika kaunti ya Karachuonyo ni miongoni mwa watu 13 waliofariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 382 huku idadi ya waliopona ikiongezeka na kufikia 8,740 baada ya wagonjwa 263 kupona.
Marian amemuacha mtoto wa wiki moja na kufikisha 8 idadi ya wahudumu wa afya waliofariki kutokana na corona.
Nairobi imerekodi visa 412, Kiambu 27, Machakos na Kajiado 17, Garissa 16, Uasin Gishu 14, Mombasa 9, Nakuru 8, Nyeri & Narok 5, Makueni 4, Laikipia 2, Muranga, Kilifi, Busia, Embu, Bungoma, Kisii, Kwale & Meru 1.
Msambao wa visa hivyo Nairobi ni kama ifwatavyo; Langata 50, Westlands 48, Dagoreti North 43, Embakasi East 37, Makadara 36, Embakasi South 35, Kasarani 25, Kamukunji & Roysambu 20, Embakasi West 18, Embakasi Central, Starehe & Kibra 16, Embakasi North & Mathare 9, Ruaraka 8 & Dagoreti South 6.