Aliyekuwa mbunge wa Garsen Danson Mungatana ameshtakiwa katika mahakama ya Kibera kuhusiana na kesi ambapo anatuhumiwa kupokea pesa kwa kutumia njia za kilaghai.
Hakimu Abdulkadir Lorot amemuachilia Mungatana na mshtakiwa mwenza kwa dhamana na ya Sh200, 000 pesa taslimu na kuagizwa kurejea mahakamani kesho asubuhi.
Mawakili wa washtakiwa wameiomba mahakama iwaruhusu kutatua swala hilo nje ya mahakama ila ombi hilo limepingwa na upande wa mashtaka.
Mungatana anatuhumiwa kumlaghai mfanyibiashara mmoja Sh70M kwa ahadi kwamba angemsaidia kupata kandarasi ya kununua vifaa vya kijeshi.