Bodi ya usimamizi wa mamlaka ya kudhibiti kawi nchini (EPRA) imemteua Mueni Mutunga kuwa kaimu mkurugenzi baada ya Mahakama kusitisha kuongezewa muda kwa Pavel Oimeke.
Katika taarifa, mwenyekiti wa bodi hiyo jaji mstaafu Jackton Ojwang’ anasema Mueni amekuwa akihudumu katika wadhfa wa katibu na pia mkurugenzi wa sheria katika mamalka hiyo.
Wiki iliyopita, jaji wa Mahakama ya kutatua mizozo ya kikazi Hellen Wasilwa alizuia bodi hiyo dhidi ya kumuongezea muda Oimeke hadi pale kesi dhidi yake itakaposkizwa na kuamuliwa.
Mkenya Emmanuel Wanjala Wamalwa kupitia kwa wakili wake Henry Kurauka anataka tume ya maadili na kupambana na ufisadi cnhini EACC kuchunguza madai ya ufisadi yanayomkabili Oimeke na kumchukulia hatua.
Kesi hiyo itaskilizwa oktoba mosi mwaka huu.