Mudavadi na Moi wapigia debe mswada wa BBI

0

Kinara wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amesema wanaunga mkono ripoti ya BBI siku moja baada ya shughuli ya kutafuta sahihi milioni moja kung’oa nanga rasmi.

Mudavadi katika taarifa kwa waandishi wa habari amesema mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali ikiwemo wao kama chama na viongozi wa kidini yamejumuishwa kwenye mswada huo na hivyo kutoa nafasi ya kujumuishwa kwa maoni yaliyotolewa.

Miongoni mwa mapendekezo ambayo Mudavadi anasema wameridhishwa nayo ni kuwanyima wanasiasa nafasi ya kuwateua makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kinyume na ilivyokuwa imependekezwa hapo awali.

Chama hicho hata hivyo kinahoji kuwa bado kuna nafasi ya kuafikia maelewano kuhusu maswala yenye utata.

Wakati uo huo

Seneta wa Baringo Gideon Moi ameongoza shughuli ya kukusanya sahihi za BBI katika kaunti ya Narok hii leo.

Mwenyekiti huyo wa chama cha KANU amepigia debe mswada huo wa BBI akisema lengo lake ni kurekebisha vipengee muhimu kwenye uongozi wa taifa hili.

Amewasihi Wakenya kusoma mswada huo na kuuelewa kwani una manufaa kwa makundi mbalimbali ikiwemo vijana.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here