Mudavadi aridhia kujiuzulu kwa Muluka

0

Kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi ameridhia kujiuzulu kwa Barack Muluka kama katibu mkuu wa chama hicho.

Mudavadi katika barua amesifia utendakazi wa Muluka alipokuwa katibu mkuu na kumtakia kila la kheri.

Muluka alisema amechukua hatua hiyo ili kumpa Mudavadi nafasi ya kujiandaa vyema kwa uchaguzi mkuu ujao.

Muluka pia amemtaka msajili mkuu wa vyama vya kisiasa kuondoa jina lake kwenye sajili ya wanachama wa ANC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here