Muda wa kuabudu waongezwa

0

Serikali imetangaza kulegeza masharti ya ufunguzi wa maabadi kuanzia Jumanne wiki ijayo.

Mwenyekiti wa baraza kuu lilobuniwa kuangazia ufunguzi wa sehemu za kuabudu Askofu Anthony Muheria amesema muda wa ibada umeongezwa kutoka saa moja hadi saa moja na nusu huku pia watoto walio na umri wa zaidi ya miaka sita na wazee wasiozidi umri wa miaka 65 wakiruhusiwa kuhudhuria ibada.

Muheria anasema idadi ya waumini kanisani italingana na ukubwa wa kanisa mradi waumini wakae umbali wa mita moja unusu.

Watu walio na magonjwa mengine na pia wakongwe walio na zaiid ya umri wa miaka 65 wametakiwa kuendelea kuabduu kutoka manyumbani mwao.

Katika hafla za mazishi, Muheria amesema pia kuwa ni watu mia moja pekee ambao wanaruhusiwa lakini mahali pa kuzikwa kwa mwili, ni watu kumi na tano pekee wanaoruhusiwa.

Muheria anasema maombi pekee ndiyo ambayo yanaweza kusaidia kuangamiza janga hili la corona ila wanawataka waumini na wakenya wote kwa ujumla kuendelea kuzingatia masharti yaliyotolewa na wizara ya afya ikiwemo kuvalia barakoa, kuzingatia usafi na kunyunyiza dawa za kuuza virusi vya corona kanisani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here