Mtu mmoja ameaga dunia na wengine wanne kujehuriwa katika ajali ya barabara iliyotokea mapema hii leo katika eneo la Kapiti, barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema ajali hiyo ilitokea baada ya gari moja kugonga nyingine kutoka nyuma na zote zikashika moto karibu na makutano ya Machakos kutokana na kile wanasema ni uetepetevu wa dereva.
Magari hayo mawili yalishika moto huku waliokuwa ndani wakisaidiwa na wapita njia kutoroka.
Waliojehuriwa wamekimbiziwa katika hospitali ya Machakos level 5 ambapo wanapokea matibabu huku polisi wakiaznisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Ajali hiyo ilisababisha msongamano wa magari katika barabara hio mapema leo asubuhi na iliwabidi maafisa wa trafiki kuingilia kati.