Mtoto wa mwezi mmoja miongoni mwa waliopatikana na corona leo

0

Mtoto wa mwezi mmoja ni miongoni mwa watu 212 ambao wamepatikana na virusi vya corona kwa muda wa saa ishirini na nne zilizopita baada sampuli 3,937 kupimwa.

Akizunguma katika kaunti ya Homabay,  katibu mkuu katika Wizara ya Afya Rashid Aman anasema hii inafikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 34, 705.

Watu 195 wamepona baada ya kuambukizwa virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 20,644 huku wagonjwa wanne zaidi wakifariki.

Msambao wa virusi hivi katika kaunti Nairobi 96, Mombasa 21,  Kiambu 11, Busia 10,Uasingishu na Laikipia 9, Taita taveta na Narok 8 ,Machakos na Nakuru 7,Kilifi na Lamu 6, Kajiado, 4 Bomet 2, Bungoma, Kericho, migori ,Muranga West pokot ,Meru na Nyeri 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here