Mtoto wa miezi mitatu ni miongoni mwa waliokutwa na corona

0

Mtoto wa miezi mitatu ni miongoni mwa watu 866 waliopatikana na virusi vya Corona kati ya sampuli 7,185 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa 87,249.

Kupitia kwa taarifa iliyotumwa na waziri wa afya Mutahi Kagwe watu 322 wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 68,110.

Wagonjwa wengine 6 wameaga dunia na kufikisha idadi ya walioaga kuwa 1,506.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 273, Mombasa 78, Nakuru 73, Kiambu 55, Kirinyaga 49 na Nyamira 35.

Takribana 1,194 wamelazwa hospitalini ni 7,984 wanashughulikiwa nyumbani huku wengine 77 wakiwa katika chumba cha watu mahututi ICU.

Idadi ya wagonjwa wanaosaidiwa na mashine kupumua ni 31.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here