Mswada wa BBI wapata sahihi Milioni 5.2

0

Kamati ya BBI imetangaza kuwa takriban sahihi milioni tano nukta mbili zilikusanywa baada ya kuzinduliwa kwa zoezi la kutafuta sahihi zinazolenga kufanyia katiba marekebisho.

Haya yamefichuliwa na kamati hiyo wakati wa uzinduzi wa nakala zilizotiwa saini kwenye hafla iliyoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.

Odinga vile vile amewasuta wanaopinga mchakato huo akisema wanafaa kuwaacha Wakenya kufanya maamuzi kuhusu hatma ya marekebisho ya katiba.

Kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na mwenzake Dennis Waweru imesema sahihi hizo zitawasilishwa kwa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa ukaguzi juma lijalo.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, wamefaulu kusanya sahihi zaidi ya milioni tano kwa sababu idadi kubwa ya Wakenya wanaunga mkono mchakato wa kufanyia katiba marekebisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here