MSHUKIWA WA MAUJI YA SHAKAHOLA AAGA DUNIA

0
MACKENZIE MAHAKAMANI

Mshukiwa wa pili wa mauaji ya Shakahola anaripotiwa kuaga dunia ingali akiwa anapokea matibabu katika hospitali moja jijini Mombasa.

Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Jami Yamina, kesi dhidi ya washukiwa wenza itaendelea huku mahakama ikisubiri taarifa rasmi.

Inaarifiwa Edison Safari Munyambo almaarufu Baba Sifa aliaga dunia siku chache zilizopita baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Haya yanajiri kufuatia kifo cha mshukiwa mwingine; Mary Charo Mbita ambaye aliaga akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Pwani.

Wawili hao walikuwa miongoni mwa washukiwa 95 ambao wanadaiwa kuhusika na vifo vya watu 283 mbele ya hakimu mkuu wa Mombasa Alex Ithuku.

Washukiwa hao wakiongozwa na mshukiwa mkuu wa mauji hayo mchungaji mwenye utata Paul Nthege Mackenzie wanakabiliwa pia na tuhuma za ukatili dhidi ya watoto, ugaidi, kutoa mafunzo ya itikadi kali, kuwa wanachama wa kikundi cha kigaidi na mauji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here