Maafisa wa polisi wamewakamata baadhi ya abiria na wamiliki wa matatu katika kaunti ya Mombasa mapema hii leo kwa kukosa kufuata masharti ya kujikinga na virusi vya corona.
Mkuu wa polisi Changamwe, Joseph Kavoo amesema zadi ya magari 100 ya uchukuzi wa umma yanazuiliwa kufuatia msako huo ulioendeshwa mapema hii leo na wamilki wa matatu hizo wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Changamwe wakisubiri kufikishwa mahakamani.
Kavoo amesema waliokamatwa hawakuwa wamevalia barakoa, na wamiliki wa matatau hawakuwa wamewapa sabuni na maji ya kunawa mikono huku wengine pia wakikosa kuzingatia sheria ya kukaa umbali wa mita moja unusu.
Amesema watapelekwa kortini baadae hii leo kufunguliwa mashtaka ya kutofuata masharti ya wizara ya afya kujikinga na virusi vya corona.