Kamati maalum ya watu kumi na mbili iliyobuniwa kutanzua mgogoro kuhusu mswada tata wa ugavi wa mapato hatimaye umeafikia makubaliano kuhusu mfumo utakaotumika kugawa rasilimali za kitaifa katika serikali za kaunti.
Ripoti ya kamati hiyo ambayo imekuwa katika mazungumzo kuanzia leo asubuhi inatazamiwa kuwasilishwa katika bunge la Senate alasiri hii kwa mjadala kabla ya kupigiwa kura.
Kamati hiyo inajumuisha maseneta Moses Wetangula (Bungoma), Johnson Sakaja (Nairobi), Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet), Mutula Kilonzo Jr. (Makueni), Ledama Ole Kina (Narok), Moses Kajwang (Homabay), Nderitu Kinyua (Laikipia), Steward Madzayo (Kilifi), Mahamud Mohamed (Mandera), Susan Kihika (Nakuru), Anuar Loitiptip (Lamu) na Samson Cherargei (Nandi).