Mkutano wa Ruto Nyamira kuendelea Alhamisi

0

Polisi wameruhusu kuendelea kwa hafla ya mchango itakayoongozwa na naibu rais William Ruto katika kaunti ya Nyamira Alhamisi wiki hii.

Kibali hicho kimepeanwa baada ya waandalizi wa mkutano huo utakaondaliwa katika uwanja wa michezo wa Sironga kuzingatia masharti yaliyotolewa na kamati ya usalama wa kitaifa.

Itakumbukwa kwamba mkutano sawa na huo ulitibuliwa na Polisi juma lililopita katika shule ya msingi ya Kebirigo na Nyaangoge huku Polisi wakilazimika kutumia vitoa machozi kuwafukuza waliokuwa wamejitokeza kuhudhuria.

Vurugu hizo lilimlazimu Ruto kuhairisha mikutano hiyo baada ya kushauriana na viongozi katika kaunti hiyo.

Wakati uo huo

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ametetea sheria zilizotangazwa na baraza la kitaifa la ushauri wa kiusalama kudhibiti mikusanyiko.

Akizungumza baada ya kuwapa vyeti wawaniaji wa uchaguzi mdogo wa Msambweni, Wudanyi/Mbale na Kahawa Wendani, Kalonzo amesema chama chake kimekuwa kikiwaandikia barua polisi kuwafahamisha kuhusiana na mikutano yao ili kuwapa kibali.

Hata hivyo Musyoka amesema shaeria hizo hazifai kutumika kwa njia ya mapendeleo na kuwataka maafisa wa polisi kuzingatia sheria katika utendakazi wao.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here