Mkewe rais Margaret Kenyatta apongeza wahudumu wa afya wa jamii

0

Mkewe rais Margaret Kenyatta amepongeza jukumu muhimu linalotekelezwa na wahudumu wa afya wa jamii katika kupambana na janga la COVID19.

Bi. Kenyatta ametaja kuwa elimu ya kutosha inapaswa kutolewa kwa wahudumu hao ili kuokoa maisha ya watu haswaa wakati huu wa corona.

Mkewe rais amesema haya alipoongoza kufuzu kwa wahudumu wa afya wa jamii wapatao 5,100 waliokamilisha mafunzo ya mwezi mmoja kuhusu kupambana na corona chini ya ufadhili wa mpango wa Beyond Zero unaogharimu Sh4.6M.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here