Mkewe rais ahaidi kusaidia kupambana na saratani

0

Mkewe rais Margaret Kenyatta ametoa hakikisho la kuendelea kuunga mkono juhudi zinawekwa na serikali za kaunti kupambana na saratani.

Kwenye ujumbe wake wakati wa ufunguzi wa kliniki ya saratani mjini Nanyuki kama mikakati inayowekwa mwezi huu wa kutoa hamasisho kuhusu ugonjwa huo, mkewe rais amesema atatumia mbio za Beyond Zero kuwapima akina mama kubaini hali yao ya ugonjwa huo.

Mkewe rais aidha amezihongera juhudi zinaendelezwa na wake wa magavana katika kuhakikisha kuwa akina mama na wasichana wanapata huduma bora za afya katika kaunti mbalimbali.

Amesema ushirikiano baina ya waandalizi wa mbio za Beyond Zero na serikali za kaunti zimewezesha kuimarishwa kwa huduma za matibabu mashinani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here