Mmarekani mzaliwa wa Kenya Huldah Momanyi ameandikisha historia kwa kushinda kiti katika bunge la wawakilishi kwenye jimbo la Minesotta.
Momanyi anakuwa mkenya wa kwanza kuchaguliwa katika bunge la Wawakilishi nchini Marekani ambayo ni sawa na bunge la kitaifa humu nchini.
Momanyi likuwa akiwania kiti hicho kwa tikiti ya chama cha Democratic Farmer Labour Party DFL.
Momanyi amepata asilima 64 ya jumla ya kura zote zilizopigwa katika jimbo hilo.
Maono ya Momanyi kwa Jimbo la Minnesota ni kuangazia masuala muhimu kama vile usalama, makazi yenye usawa na huduma ya afya inayoweza kufikiwa.
Hapo awali, akizungumza na wanahabari kuhusu changamoto ambazo amekumbana nazo wakati akiwania kiti hicho, Momanyi alifichua kuwa mhamiaji na mwanamke wa rangi kulifanya kampeni yake kuwa ngumu.
“Kuna upanga wenye makali kuwili ambapo ujuzi wangu, uzoefu, elimu kila kitu kinazingatiwa kutoka kwa mtazamo wa kile ninachojua kuwa hata umehitimu,” alifichua.
Katika mchujo wa chama cha Democratic, alipata ushindi kwa asilimia 51.28 ya kura, akimshinda mgombea mwenza Wynfred Russell.
Momanyi ni bintiye Philip na Tabitha Momanyi ambao walihamia Marekani Zaidi ya miaka 20 iliyopita angali akiwa na miaka tisa.
Mzaliwa huyo wa Kenya ana shahada tatu na shahada ya uzamili zote kutoka chuo kikuu cha Bethel.